Matumizi ya Lugha za Asili: Mfano wa Lugha ya Kirangi

Authors:
Date:
2004
Abstract:
Makala hii inachunguza nafasi zinazobaki kwa matumizi ya lugha za asili kimaandishi wakati lugha ya taifa Kiswahili hutumiwa katika maeneo mengi ya maisha ya kila siku. Lugha husika ya makala hii ni lugha ya Kirangi ambayo huongewa na wasemaji zaidi ya laki tatu katika Wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma. Tangu 1996, shirika la SIL limetoa huduma ya maendeleo ya lugha ya Kirangi; hasa, wanashirika kwa msaada wa Warangi wenyewe wameunda mfumo wa herufi, yaani alfabeti ya Kirangi, pamoja na uchapishaji wa maandiko mbalimbali. Ili kugundua Warangi wangetumia lugha yao kwa aina ya maandiko yapi, utafiti wa kiisimu-jamii ulifanyika. Wasemaji Warangi zaidi ya mia moja wameshajaza hojaji, nayo majibu yanaonyesha kwamba asilimia zaidi ya thelathini wanadai kwamba wanatumia lugha ya Kirangi kwa ajili ya kuandika, k.m. barua za binafsi. Tena, karibu nusu walisema kwamba wana hamu ya kusoma maandiko ya Kirangi kama vile hadithi za kale. Kufuatana na matokeo ya hojaji hiyo, kalenda ya mwaka 2004 imechapishwa inayoonyesha methali za Kirangi. Pia, Warangi wengine wameanza kukusanya methali nyingine na hadithi za kilugha ili kuzihifadhi kwa vizazi vijavyo. Aidha, kuna nafasi katika idara ya elimu. Kwa vile wengi wameshaandika lugha ya Kirangi katika barua za binafsi, itafaa kuboresha matumizi hayo kwa kufundisha maandishi ya Kirangi, yaani herufi zilizoundwa rasmi. Ilivyoonyeshwa wazi na Tabouret-Keller na wengine (1997), mazoezi ya kusoma na kuandika katika lugha ya asili yataimarisha uwezo wa kusoma na kuandika katika lugha ya taifa.
This paper investigates the written uses of Rangi, a minority language of Tanzania, over against the ubiquitous use of Swahili, Tanzania’s national language. It summarises the history of the Rangi language project under the auspices of SIL since 1996. Also, it reports the results of a sociolinguistic questionnaire in which 30+% of the over 100 respondents claim to write in Rangi at least occasionally.
Extent:
7 pages
Subject:
sociolinguistic questionnaire
Rangi language
minority languages
matumizi ya lugha
lugha za asili
Language use
Kirangi
isimujamii
Country:
Tanzania
Subject Languages:
Nature of Work: